Image default
Soka

Mpanzu amrushia salamu Diara, Fadlu aapa kisasi dhidi ya Yanga

ELLIE Mpanzu kiungo mshambuliaji wa Simba,amesema iwapo Septemba 16mwaka huu itamkuta katika utimamu wake kimwili na akili itakua siku ngumu kwa kipa namba moja wa Yanga Djugui Diara. Kauli ya Mpanzu imekuja zikiwa zimesalia siku 14 kabla ya kupigwa mechi ya Ngao ya Jamii baina ya wenyeji Yanga dhidi ya Simba itakayochezwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Xavi afichua siri za Elie Mpanzu | Mwananchi

Alisema,kwa sasa miguu na kichwa chake viko tayari kwa mchezo huo ambapo amepanga kumuokotesha mipira nyavuni Diara ili kuwapa furaha ya ushindi mashabiki wa Simba wenye kiu ya kuona timu hiyo inaanza vyema msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Mpanzu alisema,anatambua thamani ya jezi ya Simba ni kupata ushindi kwa kila mechi hivyo anataka kuufanya mchezo huo wa Septemba 16 mwaka huu kuingia katika historia ya maisha yake ya soka la Tanzania.

“Ukiwa mchezaji mkubwa ni lazima uwe na malengo kwa timu yako,kwangu mchezo mkubwa ulio mbele yetu ni dhidi ya Yanga hivyo natamani nifanye kile ambacho mashabiki wanataka kukiona kutoka miguuni na kichwani kwangu ambacho ni kufunga tu,”alisema Mpanzu

Fadlu anawaza kisasi tu kwa Yanga!

Kocha Mkuu wa Simba SC, Fadlu Davids, kwa sasa ana wazo moja kuu: namna ya kulipa kisasi dhidi ya mahasimu wao Yanga kuelekea mechi ya Ngao ya Jamii itakayopigwa Septemba 16 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Kocha huyo ameIAMBIA SPORTS360 Tz,kwamba,safari ya mafanikio ya Simba msimu huu inaanza na kupania..

Fadlu anatambua mashabiki wa Simba wamechoshwa na mwenendo wa kufungwa na Yanga mara kwa mara katika misimu ya karibuni. Ameazimia kuanza kwa kishindo msimu mpya wa Ligi Kuu kwa kushinda mchezo huo ili kurejesha furaha iliyopotea.

Akizungumza na Sports360 Tz, Fadlu alisema safari ya mafanikio ya Simba msimu huu inaanza sasa; wanapania kushinda mechi hiyo ili kurudisha morali kwa mashabiki na wanachama, sambamba na kujiandaa vyema kwa kampeni kubwa za kutwaa mataji ya ndani na kushindana kwenye mashindano ya kimataifa.

“Safari yetu ya matumaini inaanza na mechi ya Ngao ya Jamii. Ni lazima tuunganishe nguvu kuhakikisha tunashinda, hatua ambayo pia itatusaidia kufanya vyema kwenye mechi yetu ya kimataifa kabla ya kuingia rasmi kwenye Ligi Kuu,” amesema Fadlu.

Ameongeza kuwa Dabi ya Kariakoo haijawahi kuwa nyepesi, lakini ubora wa kikosi chake unawapa imani ya kuwarudishia mashabiki na wanachama wa Simba furaha wanayoitaka.

Related posts

How To Reduce Brain Inflammation With A Keto Diet

Chief Editor

Simba SC iko kwenye mazungumzo ya kumsajili kiungo chipukizi Paul Attah Agyei kutoka Ghana.

Chief Editor

Fadlu Davids: Na Safari Yakurejesha Heshima Simba

Chief Editor