Image default
Soka MajuuUsajili

Alexander Isak ajiunga na Liverpool kwa dau la pauni milioni 125!

Alexander Isak amesaini Liverpool akitokea Newcastle kwa uhamisho wa rekodi ya Uingereza wa pauni milioni 125 katika Siku ya Mwisho ya Dirisha la Usajili; makubaliano hayo yanazidi ile ada ya pauni milioni 115 ambayo Chelsea waliilipa Brighton kwa Moisés Caicedo majira ya kiangazi mawili yaliyopita; Isak amesaini mkataba wa miaka sita Anfield; Liverpool wametumia pauni milioni 446 kiangazi hiki.

Liverpool wamekamilisha usajili wa mshambuliaji wa Newcastle, Alexander Isak, kwa ada ya rekodi ya Uingereza ya pauni milioni 125.

Uhamisho wa Rekodi Ligi Kuu ya Uingereza (EPL)

Uhamisho huu unavunja rekodi ya awali ya pauni milioni 115 ambayo Chelsea waliilipa Brighton kwa Moisés Caicedo mwaka 2023, na unaweka kikomo saga iliyodumu kwa muda mrefu zaidi katika dirisha hili la usajili.

Usajili ghali zaidi wa Ligi Kuu ya England;

Since 2016/17
Player To From Fee
Alexander Isak Liverpool Newcastle £125M
Florian Wirtz Liverpool Bayer Leverkusen £116.5M
Moises Caicedo Chelsea Brighton £115M
Enzo Fernandez Chelsea Benfica £106.8M
Declan Rice Arsenal West Ham £105M
Jack Grealish Man City Aston Villa £100M
Romelu Lukaku Chelsea Inter Milan £97.5M
Paul Pogba Man Utd Juventus £93.3M
Romelu Lukaku Man Utd Everton £90M
Mykhailo Mudryk Chelsea Shakhtar Donetsk £88.5M
Data updated 2025-09-01

“Imekuwa safari ndefu kufika hapa,” alisema Isak

Newcastle walitangaza kuondoka kwa Isak kupitia taarifa fupi yenye maneno 37, ambayo haikumshukuru wala kutaja mafanikio yake: “Newcastle United inaweza kutangaza mauzo ya mshambuliaji Alexander Isak kwenda Liverpool kwa ada kubwa ya uhamisho inayoweka rekodi ya Uingereza. Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Sweden alijiunga na Magpies akitokea Real Sociedad mwaka 2022 na kucheza mechi 109 katika mashindano yote.”

Liverpool Agree Alexander Isak Deal With Newcastle For British Record Fee:  Report | Football News

“Imekuwa safari ndefu kufika hapa,” alisema Isak. “Lakini nina furaha sana kuwa sehemu ya timu hii, klabu hii na kila kitu inachosimamia. Ni jambo ninajivunia na ninalisubiri kwa hamu.”

“Nimefurahi kwamba sasa ni rasmi na kwamba naweza kurejea kazini. Natazamia kuwaona wachezaji wenzangu na mashabiki, na kurudi uwanjani.”

Isak akaongeza: “Nadhani nina mengi ya kutoa, na mengi ya kuboresha. Mimi ni mshambuliaji lakini daima nataka kutoa kadiri niwezavyo kwa timu—hasa mabao, lakini zaidi ya hapo pia. Nataka kushinda kila kitu.”

Jinsi Liverpool ilivyofanikiwa hatimaye kumsajili Isak

Liverpool ilikataliwa ofa ya pauni milioni 110 pamoja na nyongeza kwa ajili ya Isak mwanzoni mwa Agosti, kwani Newcastle hawakuwa tayari kumuuza nyota wao bila masharti fulani kutimizwa.

Ingawa Newcastle walisisitiza kuwa wanamthamini Isak kwa pauni milioni 150, msimamo huo ulilegea katika wiki za karibuni baada ya Isak, akiwa na azma ya kuchunguza chaguo zake, kukosa mechi zao za ufunguzi wa msimu na kusema, “uhusiano hauwezi kuendelea.”

Isak alifunga mabao 23 ya Ligi Kuu ya England kwa Newcastle msimu uliopita na akafunga bao lao la ushindi kwenye fainali ya Carabao Cup dhidi ya Liverpool huko Wembley, jambo lililomaliza kusubiri kwa miaka 70 kwa klabu hiyo kupata taji kubwa la ndani.

Newcastle ilimsajili Isak kutoka Real Sociedad mwezi Agosti 2022 kwa pauni milioni 63. Kwa jumla, alifunga mabao 62 katika mechi 109 akiwa na Magpies. Ili kumrithi Isak, Newcastle imemsajili Nick Woltemade kutoka Stuttgart na Yoane Wissa kutoka Brentford kwa ada ya pamoja inayokadiriwa kuwa takriban pauni milioni 119.

MTIRIRIKO WA MATUKIO SAKATA LA ISAK KWENDA LIVERPOOL
Norman Vincent

Julai 15: Liverpool waambiwa Isak si wa kuuza dirisha hili; wanaelekeza nguvu kwa Hugo Ekitike.

Julai 19: Isak asafiri na kikosi kwenda Glasgow, Howe anamrejesha nyumbani kwa sababu ya tetesi za uhamisho.

Julai 23: Liverpool wamtwaa Ekitike; Newcastle tayari wamemkosa Delap na João Pedro.

Julai 24: Isak aachwa nje ya ziara ya Asia kwa “jeraha dogo la paja”.

Julai 24 (baadaye): Inabainika ameiambia Newcastle anataka kuchunguza chaguo zake.

Julai 31: Ripoti zinaonyesha Isak anajifua peke yake kwenye vituo vya Real Sociedad.

Agosti 1: Newcastle wakataa ofa rasmi ya Liverpool ya £110m + nyongeza.

Agosti 2: Newcastle watoa ofa karibu £70m kwa Benjamin Šeško; Isak arejea Uingereza kutoka Hispania.

Agosti 4: Anarudi mazoezini na kuendelea kufanyia kazi kivyake.

Agosti 4 (jioni): Newcastle waongeza ofa yao kwa Leipzig huku Man United wakiingia kwenye dili.

Agosti 8: Baada ya kukosa kirafiki vs Espanyol, Howe asema wangependa Isak abaki.

Agosti 9: Man United wamsajili Šeško licha ya kutoa ofa ndogo kuliko Newcastle.

Agosti 16: Isak aachwa nje ya mechi ya ufunguzi vs Aston Villa; Howe asema “mlango bado umefunguliwa.”

Agosti 19: Isak hakuhudhuria tuzo za PFA; kupitia Instagram awashutumu Newcastle kwa “kuvunja ahadi” na kudai mabadiliko.

Agosti 19 (usiku): Newcastle wakanusha madai na kusema watamkaribisha akirejea “akiwa tayari.”

Agosti 28: Newcastle wakubali dili la Nick Woltemade (Stuttgart), likifungua njia ya kuondoka kwa Isak.

Septemba 1: Newcastle na Liverpool wakubaliana £125m; Isak asaini mkataba wa miaka 6 Anfield.

Kama umependa makala hii na nyinginezo unaweza kutufollow kwenye page zetu za Instagram na Youtube 

Related posts

What To Eat And Not To Eat When Carrying Your First Child

Chief Editor

Simba SC iko kwenye mazungumzo ya kumsajili kiungo chipukizi Paul Attah Agyei kutoka Ghana.

Chief Editor

Lassine Kouma: Moto Mpya Unaowaka Yanga!

Chief Editor