Image default
Soka

Wananchi Wapanga “Mauaji ya Sita” kwa Simba Baada ya Wananchi Day

Mashabiki wa Yanga wanaishi kwa hamasa kubwa kuelekea matukio mawili makubwa mfululizo: kwanza ni Wananchi Day, tamasha la kihistoria litakalofanyika Ijumaa, Septemba 12, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa. Baada ya shamrashamra hizo, watasubiri kwa siku nne pekee kuelekea pambano la jadi dhidi ya Simba, mchezo wa Ngao ya Jamii utakaofungua msimu mpya wa Ligi Kuu.

When she reached the first hills of the Italic Mountains

Katika mitaa na viwanja vya hamasa, mashabiki wa Yanga wamebuni neno jipya linalosikika kila kona—“Mauaji ya Sita kwa Mnyama”. Hii ni kauli ya kuashiria matumaini na imani yao kwamba timu yao itapanua rekodi ya ushindi dhidi ya Simba kutoka mara tano hadi mara sita, na hatimaye kutwaa Ngao ya Jamii.

Ali Kamwe, hivi karibuni alitangaza kauli mbiu ya msimu huu: “Tunapiga Kichwani Tu”.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu, Ali Kamwe, hivi karibuni alitangaza kauli mbiu ya msimu huu: “Tunapiga Kichwani Tu”. Mashabiki, kwa mbwembwe zao, wameichukua na kuipa tafsiri yao ya kishujaa, wakisisitiza kuwa msimu huu ni wa kuendeleza ubabe dhidi ya watani wao wa jadi.

Wanachama wa YANGA wakipiga SALUTE la KIBINGWA kwa viongozi wa Klabu kwa MAFANIKIO makubwa waliyopata ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Kwa muda mrefu sasa, Yanga imekuwa na rekodi nzuri inapokutana na Simba Sc. Zaidi ya ushindi mara tano, pia imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu kwa misimu mfululizo, jambo linaloongeza kujiamini kwa mashabiki wao. Sasa macho yote yanageukia Ngao ya Jamii—ambapo mashabiki wa Yanga wanaamini historia ya “mauaji ya sita” itaandikwa rasmi.

Raisi wa Makombe nae akaongeza;

“Miongoni mwa rekodi kubwa ambayo tunashikilia ni kucheza misimu minne bila kupoteza kwenye kombe la FA. Ni heshima kubwa na ya kipekee na pengine inaweza kuwa rekodi bora kwa sasa AFRIKA. Niwapongeze sana wachezaji na benchi la ufundi”

Mchezaji aliyefunga bao la mwisho wa ligi alisumbuliwa sana na timu nyingi. Naomba niwambie wananchi, sisi sio akademi ya kuuza wachezaji. Sisi tunataka kupata mafanikio. Tunamhitaji sana Mzize msimu huu. Ofa ya mwisho ya Mzize ilikuja ya dola milion mbili lakini tukasema HAUZWI kwa bei yoyote. Tunahitaji mafanikio hatuwezi kuuza silah zetu muhimu. Msimu huu ukiisha tunaweza kufikiria kufanya biashara” Aliongeza Raisi wa Yanga Sc Eng. Hersi Said

Related posts

What To Eat And Not To Eat When Carrying Your First Child

Chief Editor

Fadlu Davids: Na Safari Yakurejesha Heshima Simba

Chief Editor

Crash Diet to Consider If You Must Lose Weight Fast

Chief Editor