MAZUNGUMZO yanayoendelea kati ya wakala wa Simba na viongozi wa Lion Of Heart ya Ghana yanaweza kuja na habari njema kwa klabu hiyo ya Tanzania, kufanikiwa kumnasa kiungo hatari kwa kucheka na nyavu Paul Attah Agyei.
Kwa sasa Agyei anakipiha katika klabu hiyo akivaa jezi namba 7, tayari ameridhia kujiunga na Wekundu wa Msimbazi ya Tanzania endapo makubaliano baina ya pande mbili yatafikiwa. Katika kumalizia mawindo yao kwa ajili ya kupata Straika mwenye maamuzi uwanjani kama kutimiza hitaji la kocha Fadlu Davis, Simba ilipiga hodi katika klabu hiyo ya nchini Ghana na kuweka ofa nono kwa ajili ya kumnasa mchezaji huyo. Hata hivyo kuhitajika kwa Agyei na klabu ya Simba ni kama vile imetonesha mioyo ya wapenzi wa Lion Heart (Moyo wa Simba) ya nchini humo, kwa vile Agyei kwa sasa ndiye kinara wa kupachika mabao, akiwa ni mfungaji anayetegemewa zaidi kwa ufungaji mabao wa kichwa.
Fadlu amchukua Mghana kufunga usajili wa Msimbazi
Mpaka sasa ameendelea kupata jina kutokana na kuweka rekodi ya kuwafunga wapinzani wao timu kongwe ya Asante Kotoko katika mchezo wa mwisho wa Ligi ambapo Kotoko walilala bao 1-0, likiwekwa kimiani na nyota huyo anayewindwa na Simba Sc. Habari zizizopatikana kutoka ndani ya kambi ya Simba zimeeleza kuwa, mabingwa hao wa zamani wamekubali kulipa faini kwa ajili ya kuchelewa kufanya usajili ili mradi iweze kumpata mpachika mabao huyo wa uhakika hasa baada ya kocha Fadlu kuridhishwa zaidi na kiwango cha mawinga wa pande zote, lakini akiwa na hofu juu ya mchezaji atakayekuwa akifanya kazi ya kuweka mipira wavuni tu.
Amejipatia umaarufu kwa rekodi ya kuifunga Asante Kotoko kwenye mechi ya mwisho ya ligi.
Kwa sasa Simba ina Straika watatu, Jesse Mukwala, Jonathan Sowah na Selemani Mwalimu aliyekamilisha usajili wake wiki iliyipita, hata hivyo ocha alisisitiza kuhitaji mchezaji mmoja kwenye eneo hilo atakayekuwa na uwezo wa kumalizia mipira hasa ya juu. Simba ilirejea jijini Dar es Salaam wiki iliyopita,ikitokea nchini Misri ilikoweka kambi ya mwezi mmoja ikijiandaa kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu pamoja na michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Wanasimba wote ambao mmejitokeza kwenye uzinduzi wa Wiki ya Simba 2025.

